Queen Darleen Aanika Tabia Yake Mbaya

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika Kundi la WCB, Mwanahawa Abdul maaruufu kama Queen Darleen amefunguka na kuanika tabia yake mbaya.

First Lady wa WCB amefunguka na kuweka wazi kuwa, alipokuwa mdogo alikuwa chau­roho kwani alipenda sana kukomba chakula akiwa anakula na watu wengi.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Queen Dar­leen alisema alifikia hatua ya kuonekana na tabia hiyo kwani kila al­ipokuwa anakula kwenye sahani au sinia na wen­zake, alikuwa akikomba chakula na kujikusanyia upande wake.

Nilikuwa na tabia mbaya sana, yaani tukiwa tunakula wengi kwenye sinia halafu nione kama wananizidi spidi, naanza kukomba chakula, najiku­sanyia upande wangu yaani nilikuwa mroho kupitiliza, ila mama yangu aliikome­sha hiyo tabia kwa sababu ilikuwa ikitia aibu mbele za watu”.

Queen Darleen alifunguka maisha hayo aliyokulia uswahilini ‘Tandale’ pamoja na kaka yake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.