Rachel: Sijawahi Kushika Mimba Wala Kuwa na T.I.D

Msanii wa Bongo fleva Rachel Kizunguzungu aliyetamba miaka ya nyuma na nyimbo zake kama ‘Upepo’ ‘ kizunguzungu’ na nyinginezo nyingi. Rachel alianzia Sanaa yake kutoka katika Nyumba ya vipaji Tanzania (Tanzania House of Talent) THT.

Kwa kipindi kirefu Rachel amekuwa kimya kisanaa na katika kipindi hicho kuna maneno mengi sana yaliyosemwa juu yake ikiwemo ile skendo yake ilimpeleka mahabusu ya matumizi ya madawa ya kulevya.

download latest music    

Mbali na hivyo lakini pia skendo ambayo ilivuma sana kipindi hiko ni kuhusu Rachel kuwa mjamzito lakini pia inasemekana kuwa ulikuwa ni ujauzito wa msanii mwenzake wa Bongo fleva T.I.D.

Kwenye mahojiano na Enews ya East Africa Tv, Rachel amekanusha vikali tetesi hizo na kudai ni uzushi na uongo mtupu;

Kwanza naomba niseme kuwa sina ujauzito wa T.I.D wala sijawahi kushika ujauzito wake lakini pia sijawahi kushika ujauzito wowote yaani wa mtu yoyote yule alafu pia sijawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na T.I.D hata siku moja na wala haitakuja kutokea sidhani alafu nshangaa hizi habari zimetoka wapi maana mimi binafsi sijawahi kutamka kama ni mjamzito na hata kama ningekuwa mjamzito usingeweza kuwa wa T.I.D labda mtu mwingine mimi sijaamua kuwa mama kwa sasa kuna kitu natafuta kwanza ila sina matatizo ya uzazi muda ukifika nitazaa”.

Lakini pia Rachel amekiri kuwa ana mpenzi wake ambaye yuko Uarabuni ambako alikuwa ametoka hivi karibuni na kuonyesha mapenzi kwake ameamua Kuchora tatoo ya jina lake kwa lugha ya kiarabu.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.