Ramsey Nouah Amkumbuka Marehemu Kanumba

December 15, 2017 at 12:56
Ramsey Nouah Amkumbuka Marehemu Kanumba

Muigizaji maarufu wa Nollywood Ramsey Nouah amefunguka na kueleza kuwa anamkumbuka msanii wa Bongo movie marehemu Steven Kanumba kwa sababu ndiye aliyejenga daraja la ushirikiano kati yao.

Kanumba alijaribu sana kuipeleka bongo movie kimataifa zaidi kwa kutafuta wasanii mbali mbali wa nje ya nchi na kushirikiana nao iki kukuza sanaa kwa kipindi hiko.

Loading...

Ramsey amekiri kuwa Kanumba ndiye aliyewezesha ushirikiano kati ya Nollywood na Bongo movie. Yeye na Kanumba walicheza movie mbili pamoja ambazo ni Devils Kingdom na Moses..

Kwenye mahojiano aliyofanya Jana nchini Tanzania Ramsey alifunguka haya kuhusu uhusiano wake na Marehemu Kanumba:

Nimemkumbuka Kanumba ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kunileta nchini Tanzania na kushirikiana naye kwenye filamu kadhaa, sitaweza kumsahau alikuwa ni mtu mzuri aliyependa udasisi na kujifunza”.

Ramsey amekuja nchini Tanzania kwa ajili ya kushiriki kwenye kongamano la kutambua fursa kwa vijana nchini kwa mualiko wa Sahara Tanzania.

Lakini Ramsey hakuishia hapo alisisitiza kuwa siku ya Jumamosi ataenda kutembelea kaburi la Marehemu Kanumba na kuwasihi Watanzania wote waungane naye:

Nawaomba Watanzania muungane nami katika kuweka maua na kuwasha mshuma kwenye kaburi la marehemu Kanumba”.

 

Leave a Reply

avatar

in Entertainment
Loading...

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.