Ray Ameongea Haya Baada Ya Mtoto Wake Kuvunja Rekodi Mtandaoni

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Ray Vincent Kigosi amefunguka kuhusu mtoto wake na kudai kuwa ameyatoa maisha yake kwa ajili ya mtoto wake.

Ray amezaa na mpenzi wake wa Siku nyingi na sasa mzazi mwenziye ambaye pia ni muigizaji katika tasnia ya Bongo movie Chuchu Hansy. Wawili hao wamezaa mtoto wao wa kwanza wa kiume anayeitwa Jayden.

download latest music    

Baada ya kumweka hadharani hatimaye Jayden alizua balaa kwenye mitandao ya kijamii kwa uzuri wa mtoto yule ambaye amefanana copy right na baba yake Ray. Mastaa mbali mbali kama Wema Sepetu, Jokate Mwegelo na wengineo walimposti Jayden na kumsifia sana kitendo kilichopelekea mtoto huyo kutapakaa kila kona mtandaoni.

Lakini sasa Ray Kigosi amefunguka ya moyoni kuhusu mtoto wake huyo na kueleza kuwa hivi sasa Jaden ni maisha yake kwani amejitoa kwa ajili ya mwanaye na tangu azaliwe amebadilisha sana maisha yake.

Ray amelifungukia gazeti la ‘ Ijumaa Wikienda’ na kusema ameyatoa maisha yake kwa ajili ya Jaden na anafanya kazi kwa nguvu kwa ajili yake ili asije pata shida baadae kwani hatopenda mwanaye aje afanye sanaa baadae.

Kusena ukweli hivi sasa maisha yangu nimemtolea mwanangu na ninafanya kazi kwa nguvu zangu zote kwa ajili yake kwani sitopenda mwanangu aje kuwa msanii hata siku moja nataka asome ili aje kufanya kazi za kawaida”.

Ingawa watu wengi walivutiwa na uzuri na usmart alionao mtoto lakini pia wapo ambao waliwajia juu Ray na Chuchu kwa kitendo Chao cha kumtoboa masikio mtoto wao mdogo tena wa kiume. Lakini yote kwa yote mtoto ni mzuri na anaonekana na afaya njema hongera kwa wazazi.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.