Ray Kigosi: Chuchu bado Mbichi licha ya kujifungua

September 13, 2017 at 13:36
Ray Kigosi: Chuchu bado Mbichi licha ya kujifungua

Msanii wa filamu za Bongo movie Ray Vicent Kigosi amefunguka na kumwagia sifa kibao mzazi mwenzie Chuchu Hansy ambaye alikuwa anasherekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa kuwa bado ni mbichi licha ya kutoka kujifungua mtoto hivi karibuni.

Ray alifunguka hayo kupitia ukurasa wake wa instagram ya kuwa licha ya kutoka kujifungua lakini bado ni mrembo kama zamani tofauti na madhanio ya watanzania wengi kuwa ukijifungua unabadilika. Ray aliandika:

“Mzungu wangu bado mbichi utafikiri hujajifungua juzi ama kweli kujifungua sio kuzeeka, Happy birthday to you Mama Jaden Chuchu Hansy”

Pia Ray alitumia siku hiyo ya kuzaliwa kumpa shukrani ya mzazi mwenzie kwa kuweza kumbadilisha jina na kuitwa baba na kumpa heshima kubwa sana.

“Asante sana kwa kuwa mama bora kwa mwanetu Jaden hakika hakuna wa kufanana na wewe nina mengi sana ya kukwambia ila wacha siku ya leo kwenye siku yako ya kuzaliwa nikwambie haya machache nakupenda nakuthamini na kukujali, Pia nitakuwa nafanya kosa kubwa sana kama sintomshukuru Mungu kwa kunizalia mtoto mzuri na kunipa heshima kubwa ya kuitwa baba” Aliandika Ray Kigosi

Leave a Reply

5 Comments on "Ray Kigosi: Chuchu bado Mbichi licha ya kujifungua"

avatar
Sort by:   newest | oldest | most voted
Ali Hassan
Guest
Ali Hassan

Ongera sana bro

Kasri Baidana
Guest
Kasri Baidana

Tuko pamoja sana

Rosalia
Guest
Rosalia

inshaalah mungu yu pamoja nanyii

Donald Majuto
Guest
Donald Majuto

Mmependeza sana wote safi

Gabriel Mzindo
Guest
Gabriel Mzindo

Ray Kigosi hakunaga kama wewe


in Entertainment
Loading...
wavatar

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.

error: Content is protected !!
error: Content is protected !!