Recho Akana Kuingizwa Katika Madawa ya Kulevya na T.I.D

Msanii wa muziki wa bongo fleva ambae alikaa kimya kwa muda mrefu kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutokana na athari alizozipata za madawa ya kulevya , amefunguka na kuongelea swala hilo huku akisema kuwa watu wamekwa wakisema maneno mengi kuhusu yeye ilhali hakuna ukweli wa mambo hayo hata kiogo.

Akielezea kwa undani kuhusu tetesi za yeye kupotelea Dubai na kutelekezwa na mwanaume ,Recho amesema kuwa  sio  kweli na kwamba alipokuwa anaenda Dubai alikuwa ameenda katika shughulli zake za kikazi na alikuwa ana uwezo wa kujimudu na hata huyo mwanaume alimpata alipokuwa huko na walikuwa wakiishi vizuri bila matatizo yoyoyte tofauti na watu wanavyosema kuwa alikuwa akiishi maisha ya shida.

download latest music    

Recho anasema kuwa alikuwa na passport yake na wala haikuwa imeisha muda, lakini pia hakwenda Dubai na mwanaume na wala hakuwa anamtegemea mwanaume yoyote, lakini pia mwanaume aliyekutana nae Dubai hakuwahi kumtesa wala kumtelekeza.

Recho anasema kuwa mara nyingi alikuwa akikaa kimya na hakutaka kuposti kitu chochote katika mitandao kwa sababu watu wengi walikuwa wakimuuliza kwanini yupo kimya na alikwa akishindwa kuelezea sababu ya kukaa kimya kwa sababu hata yeye alikuwa anaumia sana anapokumbuka kuwa kilichomfanya mpaka kukaa kimya kwenye muziki kilikuwa kikimuumiza.

watu wengi walikuwa wanajua mimi natoka na T.I.D na ndiye alienifundisha kutumia madawa ya kulevya , lakini sio kweli .Swala mimi kutoka na tid lilianza kipindi tupo Dodoma kwenye shoo ambapo T.I.D alinipost kwenye akaunti yake tulikuwa tunaenda sehemu ya kula kwaiyo watu wakaliweka kichwani kuwa Recho anatoka na T.I.D.Lakini ukweli ni kwamba sijawahi kutoka na T.I.D kabisa.

sipendi sana kulizungumzia hili swala (madawa ya kulevya) kwa sababu nakumbuka vitu vingi na nimepoteza watu wengi sana , marafiki , kuna watu waliniaidi kazi zimepotea , huwa naumia sana.kuna kampuni ilikuwa inataka kunichukua kufanya matangazo waka -cancel na marafiki wengi wameniacha.

Recho anasema kuwa amekuwa akikaa ndani muda mrefu kwa sababu alikuwa akikaa ndani kwa muda mrefu kwa sababu watu walikuwa wakimtenga na alikuwa akijifungia ndani muda mrefu kwa sababu hata sehemu ya kuomba ela haikuwepo watu wanakupa ahadi lakini hawakupi ela.

 

 

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.