Rosa Ree Atangaza Kuachana na Uongozi Wake

Mwanadada Rosa ree ameamua kutangaza na kusema ukweli kuwa kwa muda sasa amekuwa hafanyi kazi na uongozi wake aliokuwa akifanya nao kazi , uongozi ambao makao yake yalikuwa nchiki Afrika ya Kusini.

Rosa ree anasema kuwa yeye na uongozi wake wa Dimo wamekuwa hawafanyai kazi pamoja kwa sasa kutokana na sababu ambazo haziwezi kuzuilika kwa muda na ndio maana tangu mwaka 2018 October msanii huyo amekua akifanya kazi na watu wke wa awali.

download latest music    

Hata hivyo mwanadada huyo anasema kuwa inaishukuru kampuni hiyo kwa kufanya nayo kazi kwa kipindi walichokuwa pamoja ingawa pia kufanya kazi pekeyake kumemfanya kuwa imara zaidi.

Rosa anasema kuwa tangu ameachana na kampuni hiyo  mpaka sasa ameweza kutoa nyimbo mbili ya banjuka pamoja na asante baba ambazo pia zimekuwa zikifanya vizuri kwa sasa.

Rosa ree alitangaza kuwa katika mkataba na Dimo kwa miaka 3 ikiwa mkataba huo ungeanza kufanya kazi March 2018.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.