Rosa Ree Azidi Kung’ara Nchini Afrika Ya Kusini

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na miondoko yake ya kipekee ya kuchana Rosary Robert Kimario maarufu kama Rosa Ree ameendelea kung’aa Zaidi Sauzi.

Rosa Ree ambaye mwezi uliopita alisaini mkataba mnono na kampuni ambayo inasimamia kazi zake ya  Afrika ya Kusini imeendelea kumsimamia kazi zake vyema na hata kumtangaza zaidi nchini humo.

download latest music    

Rosa amesemekana kuwa gumzo nchini humo kutokana na Media Tour anayefanya nchini humo ambapo mbali na kuzungumza Kizungu lakini kwa kiasi kikubwa amekuwa akizungumza Kiswahili, ili kuonyesha kwamba ni Mtanzania, lakini pia amefunguka kwamba kwa sasa kazi zake kwa kiasi kikubwa atakuwa anafanyia nchini humo kwa sababu menejimenti yake inatoka huko.

Kiukweli Sauz kwa sasa kumekuwa kama nyumbani, ninafanya ziara nyingi kila kukicha na menejimenti yangu imenitengenezea mazingira mazuri ya kufanya kazi. “Baada ya kumaliza tour kuna kitu kikubwa pia kinakuja, mashabiki wangu wakae mkao wa kula”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.