Rose Ndauka Afungukia Mapenzi Yake na Dj Ommy

Muigizaji wa Bongo movie Mrembo Rose Ndauka ameibuka na kufungukia taarifa za kuwa Kwenye Penzi Zito sana na Mtangazaji na Dj maarufu Dj Ommy Crazy.

Tetesi za Rose Ndauka kuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi na Dj Ommy zilianza baada ya picha za wawili zilizoqaonyesha wakiwa pamoja kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Amani, Rose alisema hamna chochote kinachoendelea kati yake na DJ Ommy zaidi ya kuwa marafiki wanaosapotiana katika kazi hivyo kwenda kwake kwenye bethidei yake hivi karibuni kulikozua maneno lilikuwa ni jambo la kawaida tu na si vinginevyo;

Sina mahusiano na huyo mtu, mimi nilienda kwenye bethidei yake kama rafiki yangu tu na hakuna kingine. Nashindwa kuelewa hivi vitu vinatoka wapi? Wanataka mtu asimsapoti rafiki wa kawaida?“.

Tetesi hizi zinakuja kwani kwa muda mrefu Rose amesemekana kuwa Kwenye Mahusiano na mwanaume ambaye ni mdau Kwenye mambo ya siasa lakini amekataa kumtaja mtu huyo.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.