Sababu Ya Ndoa Nyingi Za Sasa Kuvunjika.

Ndoa nyingi sasa zimekuwa zikivunjika kwa sababu tu watu wamekuwa hawana  uhalisia wa maisha yao ya kawaida kwaio wanapokutana ndani katika ndoa kila mmoja anashangaa kuona mwenzie amekuwa mpya kitabia, wakinadada wengi wamekuwa na maisha ya kuigiza, hii  simaanishi kuwa wakina kaka hawapo hivyo lakini wakina dada wamezidi kwa hilo.

Kwanini ndoa nyingi za sasa zimekuwa zikivunjika , ni kwa sababu ya kufeki maisha katika vitu vifuatavyo.

download latest music    

Uvaaji.

Mnapokuwa  katika kipindi cha mahusiano mwenzi wako alikuwa akipenda kuvaa mavazi ya staa na heshima sana, kumbe alikuwa katika hatua za kutafuta ndoa.Ikifikia mpo ndani sasa na mmeshafunga ndoa kwaio ameshakipata kile alichokuwa anakitaka  mnaanza kushangaana, kama ni mwanamke ataanza kuvaa vinguo vyake vya ajabu , vifupi au mwanaume anaacha kuwa nadhifu mpaka mnaanza kupigizana makelele kwenye swala hilo.

Namna ya kuongea.

Wapo baadhi ya watu ujifanya sio waongeaji sana katika kipindi cha urafiki na ujifanya ni watu wa kusikiliza na kutenda zaidi kuliko kitu chochote kumbe ni  hatari midomoni, sasa hapo unaanza kuona mabadiliko mkifika ndani anaanza kuonyesha makucha yake  kwa mwenzi wake mpaka anafikia hatua ya kujuta na kushangaa mdomo huo ameutoa wapi.

Swala la utii.

Hakuna asiependa kusikilizwa na mwenzie, au kuonyeshwa utii na yule anaempenda, ni bora zaidi kuwa na tabia zako ili kama mtu anakupenda na kukubali kuwa na wewe katika ndoa basi awe ameshakubaliana na kila kitu, sio mnaingia katika ndoa mwanamke anaanza kuwa anajibu ovyo, hasikilizi yale anayoambiwa, hapo ndoa haiwezi kudumu hata mara moja.

Matumizi.

Hapa napo watu wengi wanakuwa wanashindwana kwa sababu mkiwa na urafiki kabla ya ndoa mtu anakuwa na matumizi ya kubana na kufanya bajeti sana na hata wakati mwingine ukimpa ela anaweza kuikataa kwamba tuifanyie kitu fulani ambacho wote mtakiona na maana ,lakini ikitokea sasa mmekaa ndani anaanza ufujaji wa mali na fedha.

Swala la faragha.

Ukweli itabidi ubaki kuwa ukweli, kama una kasoro fulani katika jambo ilo ni bora likaonekana mapema ili mwenzi wako haweze kujua ni namna gani mnaweza kulitatua, kuna watu wamekuwa wakifoji jinsi ya kushughulika anapokuwa faragha, anajituma na majonjo yote, mkifika kwenye ndoa sasa  yeye ndo mvivu wa kwanza mpaka mtu anashangaa labda unamwa au kuna kitu kimekupata kumbe hakuna lolote.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.