Sababu za Wanaume Kupenda Wake za Watu.

Kumekuwa na tabia ya wanaume wengi kutaka kuingia katika mapenzi  na wanawake mambo tayari wameshaolewa na hivyo hivyo kwa mabinti kutaka kuwa  na mahusiano na wanaume za watu bila kuogopa kuwa kitu hicho kinaharibu mahusiano ya ndoa ya watu hao au kuvunja familia kabisa.

Kwa bahati mbaya zaidi  kwa maisha ya sasa hivi kuhusu mahusiano unaweza kukutana  na mwanamke naye licha ya kwamba ameolewa lakini naye anajihisi kumpenda mwanaume huyo na  sababu kubwa huwa ni kwamba anakuwa  hapati kile ambacho alikitarajia kwenye ndoa yake. Na hi uwaweka wengi katika njia panda, lakini sababu kubwa ya watu kutembea na watu waliopo katika ndoa huwani :-.

download latest music    

PENZI LA DHATI

Baadhi ya wanaume si kwamba wanaonyesha kuwa wao hawajatulia kwa kuwatokea wake za watu. Baadhi yao penzi la dhati walilonalo dhidi ya wale ambao wameshaingia kwenye ndoa ndilo huwasukuma kufanya hivyo.

Wanachokifanya wao ni kueleza hisia zao bila kujali kuwa, mlengwa ana mtu au laa. Ndiyo maana mtu huyo anaweza kuwa anajua ukweli kwamba fulani ni mke wa mtu lakini kwa kuwa anaamini huyo ndiye wake, analazimika kujaribu zali.

Siyo dhambi kueleza hisia zako lakini ndugu yangu kama unajua kabisa huyo uliyempenda yuko ndani ya ndoa yake au ana mpenzi wake, pambana na hisia zako. Jizuie kwani kumpa usumbufu mke wa mtu ni kujitafutia matatizo bure.

HAKUNA GHARAMA

Baadhi ya wanaume wanawatokea wake za watu kwa kuwa hawatapata usumbufu wa pesa za matumizi, vocha, mavazi na vitu vingine. Wao wanaamini watakuwa wanatoa penzi tu lakini mambo mengine mwenye mke atahudumia.

Lakini wengine wanataka kuanzisha uhusiano na wake za watu kimaslahi. Kwamba mwanaume anaweza kuona mwanamke flani ameolewa na mwanaume mwenye nazo lakini mke anaonekana kutopata penzi analolihitaji. Yeye anatupa ndoano, akiamini akimridhisha kimapenzi, atakuwa anahongwa yeye na maisha yake yatakuwa poa.

Tahadhari. Kama unatokea kumpenda mke wa mtu ili umchune au ili kukwepa kugharamia, tamaa yako hiyo itakuponza. Acha utegemezi, mwanaume aliyekamilika ni yule mwenye uwezo wa kumtunza mtu anayempenda, usikimbie majukumu na kutaka vya mteremko. Kumbuka wengi walioingia kwenye uhusiano na wake za watu kwa tamaa za pesa na mali, yamewakuta makubwa.

USUMBUFU HAKUNA

Kuna wanaume ambao hawapendi kusumbuliwa kwa mambo ya wivuwivu na wapenzi wao, mara nyingi mwanaume anapoanzisha uhusiano na mtu ambaye ana mtu wake anahisi hatasumbuliwa.

Yale mambo ya; ‘uko wapi baby’, uko na nani, nataka tuonane leo’ yanakuwa si kwa kiwango kile ambacho kinakuwepo kwa mtu ambaye hana mtu.

HAKUNA KUGANDANA

Wapo wanaume ambao wao wanataka kila mwanamke mzuri bila kujali ameolewa au yuko singo. Lakini pia wapo ambao hawataki kuingia kwenye uhusiano na mwanamke ambaye atagusia future. Kwa kifupi wanaume wa staili hii wanaamini wakiwa na wake za watu, hawawezi kugandwa wala kuulizwa juu ya ‘future’.

SIFA TU

Wapo wanaume ambao wakitembea na mke wa mtu wanaona sifa sana. Akimtongoza mke wa mtu, akakubaliwa, roho yake inakuwa fresh. Na wengine hawawezi kubaki na siri, kila atakayekutana naye atamwambia; ‘yule mbona nishampitia’.

Hiyo yote sifa. Mtu yuko tayari kutumia gharama yoyote ili mradi atembee na mke/ mpenzi wa mtu, aandike historia kwamba fulani licha ya kwamba ni mke wa mtu lakini ameshatembea naye

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.