Loading…

Saida Karoli awakanya wasanii wa kike

September 13, 2017 at 10:21
Saida Karoli awakanya  wasanii wa kike

Msanii wa kike wa bongo fleva kutoka Tanzania  ambae kwa muda mrefu alikuwa kimya , lakini sasa amerudi kwa kishindo kikubwa, Saida karoli  amefunguka na kuongea na wasanii wenzie wa kike kuacha tabia ya kujikweza na kujidai,kusifia na kujiona wao ndo wao  ,na hakuna mtu mwingine zaidi yao,saida amesema kuwa wasanii wa kike ni lazima wawe na discipline katika kazi zao kwa sababu haujui ni nani atakae kusaidia baada ya kuanguka katika kazi na maisha kwa ujumla na kwa ujumla tabia ya kufanya hivyo inakera watu wengi.

Akizungumza na mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha East Africa  msanii saida karoli anasema kuwa katika maisha kuna safari ndefu sana ivyo wasanii wanapaswa kuwa makini katika kuongea na kuishi na watu vizuri.

Loading...

“kwakweli ilo swala ni kero sana, na kero sio kwangu tu bali  hata kwa jamii kwa ujumla wake, kwasababu tabia iyo inakufanya unashuka ghafla katika kipaji chako, mtu unapokuwa ma upendo na pia hujisikii na unaongea na watu vizuri wale uliokuwa unaongea nae siku za nyumba ndio hao watakao kusupport n kukubeba pale unapoanguka” ameongea saida karoli . Hata hivyo kwa msanii  mkongwe kama Saida Karoli   kuongea na kuwaasa wasanii wa kike kuhusu swala  ilo inaonyesha kuwa alishaona baadhi ya wasanii hasa wa kike wenye tabia hizo , huu ni muda sasa wa wasanii hao  kuanza kubadilika na kuishi vizuri na wasanii wenzao na jamii kwa ujumla

Msanii Saida Karoli  ni moja kati ya wasanii wakongwe Tanzania , maarufu sana na  alikuwa anatamba na vibao kama chambua kama karanga  kipindi  cha nyuma kidogo lakini  baadae alianguka kimuziki ila sasa amerudi tena kwa kasi na kishindo kikubwa baada ya lebel ya wasafi kumsaini katika lebel iyo na kusimamia kazi zake na sasa hivi anatamba na vibao vyake  vipya kama orugambo  na kichaka aliomshirikisha gnako na belle 9 na nyimbo izo zinafanya vizuri kila kona

Comments

  1. Apambane na hali yake kila mtu na maisha yake

  2. Ni ukweli namkubali sana Saida

  3. Wadada wa bongo wana maringo hasa sn wakati huu wa instagramu,utakuta mtu ajiona queen wakati ni wa kawaida sana,inakera

  4. umefanya busara kuongea mama

  5. Dingi wa Kariakoo : September 13, 2017 at 10:55 am

    Sasa wataka tufanyeje?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment
Loading...

#Godseeker,
I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.