Loading...

Salama Jabir Kurudi Kwenye Tv Yako Na Kipindi Hiki

February 22, 2018 at 07:01
Salama Jabir Kurudi Kwenye Tv Yako Na Kipindi Hiki

Mtangazaji maarufu wa kipindi cha ‘Mkasi’ Salama Jabir alijipatia umaarufu zaidi kipindi cha nyuma kitokana na kuwa Jaji katika kipindi cha mashindano ya kusaka vipaji vya kuimba cha ‘ Bongo Star Search’.

Salama alijipatia umaarufu kama jaji kutokana na umahiri wa kusema ukweli na kuwapa makavu libe washiriki ambao walikuwa hawajui kuimba tofauti na majaji wenzake wengine kama Madam Ritha na Master Jay.

Loading...

Baada ya ukimya mrefu hatimaye Salama anarudi Tena kwenye Tv na safari hii anarudi na kipindi cha ‘Shabiki On Saturday’ ambacho kitajikita katika kuelezea stori za mashabiki kabla na baada ya mechi  ambazo mara kwa mara huwa na nakshi naskhi nyingi kuliko hata makocha na wachezaji na mara nyingi huwaacha waliofungwa wakiugulia na walioshinda wakifurahia.

Ndani ya kipindi hiko kuna mambo mengi ikiwemo mtazaamaji kupata fursa ya kupiga stori za timu yako kuanzia mechi iliyopita hadi ijayo bila kusahau  nafasi ya wewe kushiriki kwa kuonyesha uwezo wa kucheza mpira kwa Kupitia challenge.

Salama aliandika ujumbe huu kwenye page yake ya Instagram ili kualika mashabiki kutazama kipindi hiko:

Basi bwana, mapenzi yangu na mpira nikaona yasiishie tu kwenye timeline yako ya social media, Kwenye Tv yako yanaweza kuleta maana zaidi….So nikualike rasmi kwenye kipindi changu kipya cha kwenye Tv kinachoitwa Shabiki On Saturday kitakachorushwa East Africa Tv”.

 

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…