Sanchi Afungukia Biashara Ya Mbwa Inayomuweka Mjini

Mwanamitindo maarufu kwenye mitandao ya kijamii anayezidi kutesa na umbo lake matata Janey Rimoy maarufu kama Sanchi amefunguka na kuweka wazi Jinsi biashara yake ya kuisaliti mbwa inavyomuweka mjini.

Sanchi amedai kuwa anashukuru anamaliza mwaka akiwa anaendelea na maisha yake vizuri huku madili yake ya biashara ya mbwa aina ya bull yakiendelea kumfanya atanue kinoma mjini.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Sanchi alisema kuwa watu wengi wamekuwa hawamuelewi anapokuwa akipiga picha na mbwa, lakini ni kwa vile hawajui mbwa hao wanampa madili kwa kiasi gani.

Maisha yangu yanaenda kama kawaida kwa ajili tu ya hao mbwa wanaowaona kwenye ukurasa wangu wa Instagram. Mimi ni balozi wa biashara hiyo hivyo riziki yangu ya kila siku inapitia hapo”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.