Shaffie Werru Afunguka Kuhusu Ndoa Ya AY na RemmyRwanda

                                         

Msanii mkongwe wa muziki bongo Ambwene Yesaya  amefunga ndoa wikiendi  hii na mpenzi wake wa siku nyingi remmy kutoka rwanda na kufanya harusi fupi iliyokuwa ya siri na kuarikwa watu wachache wa karibu  na familia hizo.habari hizo zilianza kuvuja katika mitandao kipindi ambacho harusi hiyo ikiwa imeshafanyika na kuonekana ni watu wachache tu kutoka Tanzania na nchi rafiki waliohudhuria harusi hiyo.

download latest music    

Moja ya wahalikwa katika harusi ya msanii AY ni mtangazaji maarufu wa radio nchini Kenya Shaffie Werru ambae alitoa siri ya kualikwa kwake katika sherehe hiyo ya msanii huyo  mkongwe.Shaffie anasema kuwa tangu mwanzo alishajulishwa kuwa msanii AY alitaka ndoa yake iwe ya siri na isiwe na watu wengi hivyo waliamua kuweka wageni wachache tu na yeye akiwepo.

nimemfahamu AY kwa zaidi ya miaka kumi sasa kupitiakazi yangu hii ya utangazaji,tumekuwa tukifanya kazi pamoja kwa muda mrefu sasa,tumefanya biashara pamoja na hata kusafiri mara nyingi.AY amenisaidia kunitambulisha sana nchini mwao na mimi nimekuwa nikimtambulisha na kumtangaza sana nchi kwetu kwa muda mrefu sasa na hii ni sababu kubwa sana ya yeye kunialika mimi katika ndoa yake kama mmoja wa wanafamilia.

Katika harusi hiyo  wawakilishi wachache walioonekana kutoka Tanzania ni pamoja na rafiki wa karibu wa msanii AY ,  ni Mwana Fa, B-Dozen na rafiki wengne kutoka nchi mbalimbali.Wasanii mbalimbali walimpongeza AY kwa tukio hilo la kuchukua jiko akiwepo Profesa Jay, Diamond Platinumz na Jokate Mwegelo.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.