Shairi la Suma Lee Kuhusu Kifo cha Jeby

Mwanamuziki Suma Lee ambae alikuwa akifanya kazi za kisanii na marehemu jeby ameandika shairi rfu kuhusu kifo huku akilenga shairi ilo kwa msanii mwenzake na watu wote kwa ujumla kujua nini maana ya kifo.

Jeby ambae alifariki wikiend hii na kuzikwa huko kwao Dodoma siku ya jumatatu, alikuwa akisumbuliwa na kuishiwa na damu kwa muda mrefu.

download latest music    

INNA LILLAH WA INNA ILAIHI RAAJIUUN
#JEBBY

UNAVYO JIHISI KIFO.
Mtu huwa hatambui kuwa amekufa pale anapokufa. Yeye hujihisi anaota anakufa, anajihisi analia, anaoshwa, anafungwa na anateremshwa kaburini. .

Bado anajihisi kuwa anaota anapofunikwa na mchanga. Kisha hulia kwa makelele na hakuna anae msikia.
Baadae kila mtu anapotawanyika na ameachwa pekee chini ya ardhi, Mungu huirudisha roho yake. Anafungua macho na kuamka kutoka “ndoto yake mbaya” .
Mwanzoni, hufurahi na kushukuru kuwa alikuwa anaota tu, na sasa ameamka kutoka usingizini. Kisha hujigusa mwili wake ambao utakuwa umefunikwa na kitambaa cheupe,na kwa mshangao hujiuliza “shati/gauni langu liko wapi?”
Kisha ana anza kujihisi “niko wapi?” “hii ni sehemu gani?” Mbona kuna harufu ya udongo kila mahali? Ni nini haswa ninacho kifanya hapa?
Hapo ndipo atakapo anza kugundua kuwa yuko chini ya ardhi na alicho kihisi haki kuwa ndoto!
Ndiyo, anagundua kuwa ni kweli yeye amekufa, na amezikwa. .

Anapiga kelele kadri anavyoweza kuwaita watu waliokuwa karibu nae ambao wangeweza kumuokoa:
“baba”
“mama”
“kaka”
“dada”
“rafiki”

Hakuna anaemjibu. Kisha anagundua kuwa Allah ndio tegemeo lake pekee. Akilia na kumuita huku akimuomba msamaha :
“Yaa Allaaaaah…
Yaa Allaaaaaah…
Nisamehe mimi
Yaa Allaaaaaah!!! .

Anaita akiwa na hofu kubwa,ambayo hakupata kuwa nayo alipokuwa hai . .

Kama alikuwa mtu mwema na mcha Mungu, malaika wawili wakiwa na uso ulio na furaha watamkalisha na kumliwazana kumhudumia vizuri. .

Kama alikuwa mtu mbaya na hakuwa mcha Mungu, malaika wawili watamwongozea hofu yake na kumpa mateso kufuatana na amali zake mbaya. .

Ewe Mola, nisamehe dhambi zangu, dhambi za baba yangu, mama yangu, mke/mume wangu na wanangu na jamaa zangu na marafiki. .

Ewe Allah, usiuchukue uhai wangu ila pale nitakapo kuwa tayari kukutana nawe.

Kaka na dada katika uislam,una chaguo mbili hapa:

#1.Uache ilimu hii hapa isomwe na hakuna kitakacho tokea.

#2.#TAg Isambaze ilimu hii kwa marafiki zako,.na wote wengine.
In Sha Allah itakuwa na manufaa kwao, na wewe utafaidika

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.