Shamsa Awaasa Wanawake Waolewe Waache Kusubiria Wanaume Matajiri, Waige Mfano Wa Shilole

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford amefunguka na kuwashauri wanawake waige mfano wa Shilole na kuolewa badala ya kukaa na kusubiri kuolewa na mwanaume tajiri.

Shamsa aliongea hayo alipokuwa anampa hongera Shilole baada ya ndoa yake na Uchebe. Shilole aliolewa wiki iliyopita na Uchebe ambaye ni fundi magari na kusababisha watu wengi kumsema.

download latest music    

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Shamsa Ford alifunguka yafuatayo:

Hongera mamy umefanya maamuzi sahihi ya kumpendeza mwenyezi Mungu cha muhimu uwe mke bora wa Kitanzania kwa mumeo na ustar uweke pembeni mumuweke Mungu mbele, uvumilivu na kuheshimiana Inshallah mtazikana karibu kwenye chama mama…Sasa nyie mnaosubiri matajiri wawaoe wakati hao matajiri wana wake zao wameanza nao moja mtasubiri sana mpaka uso utaota sugu uzuri na ustar una mwisho wake itafika kipindi hata nzi hatokusogelea”.

Ingawa Shamsa hakutaja majina lakini dongo like aliliekekeza kwa wasanii wenzake ambao hawataki wanaume kuolewa na wanaume wa kawaida bali nia yao ni kupata wanaume wenye pesa lakini wanaume wale wenyewe wanawaita madanga wengi wako wameoa tayari na wanafamilia zao

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.