Shamsa Ford Adhamiria Kuachana na Nguo Za Nusu Uchi

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Shamsa Ford amefunguka na kuweka wazi kuwa moja ya mipango yake ya mwaka mpya wa 2019 ni kustaafu kabisa kuvaa vimini.

Shamsa amesema kuwa ameamua kuacha nguo za nusu uchi na kuanza kuvaa kwa stara zaidi na amedhamiria kuwabadili wanawake wengine kwa kuhakikisha anauza nguo za stara tu dukani kwake.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Shamsa alisema anamshukuru Mungu kuuona mwaka huu akiwa mzima na kwa kuwa mwaka mpya unakuwa na mambo mapya, yeye ameamua kubadilika katika suala la mavazi.

Sina sababu tena ya kuendelea kutojistiri kwa sababu Mungu ameniokoa na kunistiri kwa kunipa mume, mwaka huu ni wa kuonesha kuwa mimi ni mama mwenye stara, naamini kwa kuwa na duka la madira na mitandio nitaweza kuwa mwanamke mwenye stara na hii ndiyo njia pekee ya kunipa mwisho mwema hapa duniani“.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.