Loading...

Shamsa Ford Atishia Kumpeleka Baba Watoto Wake Kwa Makonda

April 16, 2018 at 13:07
Shamsa Ford Atishia Kumpeleka Baba Watoto Wake Kwa Makonda

Msanii wa Bongo movie Shamsa Ford amefungukia mipango yake ya kumbruza kwa Makonda Ex wake ambaye amezaa naye mtoto mmoja.

Shamsa ameweka wazi kuwa atampeleka mzazi mwenzie Dickson Matoke kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda kwa ajili ya kudai haki ya kuhudumiwa mtoto wake.

Loading...

Wiki iliyopita Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda alitangaza kuwa wamama wote waliotelekezwa na wanaume waliozaa nao waende ofisini kwake kwa ajili ya kuangalia msaada wa sheria watakaopata.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Risasi Jumamosi, Shamsa alisema kuwa sio kwamba hana uwezo wa kumhudumia mtoto wake lakini kuna wakati unaumia kuona baba wa mtoto yupo, anakula bata tu akiwa hajui hata kula ya mtoto wake inatoka wapi.

Dawa ya wanaume wa sampuli hii ni kuwapeleka tu kwa Makonda. Mimi watu watashangaa sana siku watakaponiona pale lakini ni kwa sababu wakati mwingine ukifikiria unajikuta unapatwa na hasira kuona mzazi yupo lakini kama hayupo vile”.

 

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…