Shamsa Ford Awamwagia Povu Wanaume Wanaonyanyasa Wake Zao

Muigizaji wa filamu za Bongo movie nchini Shamsa Ford ameibuka na kuwatolea Povu zito wanaume ambao wamekuwa na tabia za kunyanyasa Wake zao kwa kuwapiga.

Shamsa ametoa maneno makali ya kukemea wanaume ambao wanawafanyia vituko Wake zao Kama kuwapiga na kuwadhalilisha lakini pembeni wana michepuko wanayoithamini.

download latest music    

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameandika maneno haya:

Wanawake ambao tuna mapenzi ya dhati ndio huwa tunaonewa sana. Wanawake ambao huwa tunaishi maisha ya uhalisia kutokana na mifuko ya waume zetu ndio tunaonewa na kuonekana kama washamba, lakini wale wanawake wachunaji ndio huwa wanapewa kipaumbele na kuthaminiwa sielewi wanaume huwa wanataka nini kutoka kwa wanawake.

Tunapigwa, tunasemwa vibaya, tunaonewa, tunabeba mzigo mkubwa lakini mwisho wa siku bado unafuta machozi na kusema Alhamdulilah. Nyie wanaume huwa mnataka nini?”.

Shamsa hataweza wazi Kama ujumbe huo umeilenga ndoa yake pia na mfanyabiashara Chid Mapenzi ya la ila ameambatanisha na picha akiwa amejeruhiwa jicho.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.