Loading...

Shilole ametaja sifa za Mwanaume anaempenda

May 19, 2017 at 16:28
Shilole

Kuna fununu zinazodai kuwa Shilole amepata mpenzi ambaye anataka kumuoa lakini jambo hili halijamsimamisha kutaja sifa ambazo anazozipenda kwa wanaume.

Akizungunza hivi karibuni msanii huyu wa nyimbo za Bongo alisema kuwa yeye anawapenda wanaumbe ambao wanajitambua na ambao ni warefu ikiwa ni jambo la muonekano. Ingawa aliendelea kusema kila mtu ameumbwa vitofauti, Shilole aliweka wazi kuwa hawezi kutoka na mtu ambaye ni mfupi. Alisema,

“Mimi napenda mwanaume yoyote yule ilimradi anajitambua basi, suala la muonekano hilo linatengenezwa ila kiukweli kabisa mimi napenda mwanaume mrefu, mwanaume mfupi kwangu hapana,Sipendi Wanaume wafupi, Barnaba yeye ni mfupi na kila mmoja ameumbwa na Mungu tofauti, ila sasa hivi vigezo na masharti kuzingatiwa“

Shilole alisema haya kwenye kipindi cha Kikaangoni cha EATV huku akiongezea kuwa anatamani kuoleka kwani hii ni ndoto ya kila mwanamke.

“Hamna mtu asiyependa kuolewa, ndoa ni heshima ndiyo maana unasikia watu wanasema mke wa fulani yule, muwe wa fulani yule lakini siyo aah yule si mwanamke tu kwa hiyo ndoa ni heshima”

Leave a Reply

Be the First to Comment!

avatar
wpDiscuz

in Entertainment
Loading...
I write entertainment stories as well review and critic local music. Apart from my busy schedule you can catch me on social pages by clicking on them below