Shilole Amtolea Povu Nuh Mziwanda na Kudai Anataka Kumgombanisha na Mpenzi Wake

Mwanamuziki wa Bongo fleva Shilole amemjia juu aliyekuwa mpenzi wake Nuhu Mziwanda na kudai kuwa anataka kumuharibia uhusiano wake na mpenzi wake Uchebe.

Siku ya Jana habari zilienea kuwa Shilole amerudiana na Nuhu Mziwanda na kumuacha mpenzi wake Uchebe. Siku chache zilizopita Uchebe na Shilole walitangaza kuwa wanatarajia kufunga ndoa hivi karibuni na kudai kuwa wanataka kufunga ndoa yao Ulaya. Pia Shilole alimpeleka Uchebe Nyumbani kwao Tabora, Igunga ili kumtambulisha kwa wazazi wao.

download latest music    

Hivyo Jana baada ya habari kusambaa kuwa Shilole kamuacha Uchebe na kurudiana na Nuh Mziwanda watu wengi walishangaa kwani ni juzi tu habari zilisambaa kuwa Nuh Mziwanda amerudiana na make wake Nawal ili wamlee mtoti wao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Shilole amekataa vikali tetesi hizo za yeye kuachana na Uchebe na kurudiana na Nuh Mziwanda na hata kumnyooshea kidole Nuh na kudai kuwa yeye ndiye aliyesambaza habari hizo za uongo na ile picha ili mradi tu amgombanishe na mpenzi wake Uchebe.

Shilole ametoa tamko lifuatalo kutokana na tetesi hizo:

Ulizani utanikomoa kwa taarifa yako hiyo picha sio ya leo unaunga unga matukio ili kunigombanisha na mchumba wangu? Mashabiki zangu niwaambie tu hiyo staili ya nywele nadhani mnajua kuwa napenda kuitumia. Alipangalo Mwenyezi Mungu binadamu hawezi kulipangua”.

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.