Shilole Awajia Juu Watu Wanaoiponda Ndoa Yake na Uchebe

Msanii wa Bongo movie Zuwena Ashraf ‘Shilole’ amewajia juu watu wote walio kifua mbele kuisema na kuiponda ndoa yake na Uchebe.

Shilole na Uchebe walifunga ndoa ya siri wiki iliyopita iliyofanyika Nyumbani kwa Meneja wa Diamond Babu Tale na kugudhuriwa na watu wasiopungua kumi.

download latest music    

Tangu ndoa hiyo imefungwa kuna maneno mengi yameibuka mitandaoni hasa kwa sababu kuna ripoti zilizodai kuwa familia ya Shilole haikukubaliana na ndoa hiyo hadi kufikia hatua ya ugomvi mkubwa kutokea kati ya Shilole na Dada yake hadi kufikia hatua ya kupelekana polisi.

Baada ya maneno kuzagaa mtandaoni kuhusu Ndoa hiyo Shilole ameibuka na kudai kusikitishwa na habari za majungu zinazoendelea kusambaa kumhusu mume wake Uchebe:

Kwenye mahojiano na gazeti la Mtanzania Shilole amezidi kufunguka haya:

Mfa maji haishi kutapa tapa , Ndoa yangu imewaumiza wengi wasionipenda, nimeona maneno mengi ya kashfa na majungu wakinichafua sasa mimi nasonga mbele na maisha yangu sina habari na mtu”.

Lakini pia Shilole ameeleza kuwa pamoja na kwamba watu wanamchafua lakini anaamini ndoa yake itadumu na kwa sasa familia yake ipo vizuri na ndoa yake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.