Shiloleh Kufuata Nyayo za Mzee Yusuph

Mwanadada Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amefunguka na kusema kuwa kadri siku zinavyokwenda anaona kama inawezekana yeyekufuta nyayo za moja ya msanii mkubwa wa taarab aliyepita ya kuachana na muziki na kufanya mambo mengine ya kijamii.

Akiongea katika futari iliyoandaliwa na msanii mwenzie Iren uwoya pamoja na mumewe dogo janja anasema kuwa kwa jinsi mwezi huu mtuklufu ulivyomfunza mengi anaona kabisa kuwa hana muda mrefu anaweza kupiga chini muziki na kufanya vitu vingine.

download latest music    

si unaona ninavyopendeza na vazi hili la kiislamu,basi kwa taarifa yako sina muda mrefu na mimi nitaacha muziki kama alivyofanya Mzee Yusuf

Kikubwa na kizuri ni kwamba nina vyanzo vingine vya kimapato,unajua kuwa nina ule mgahawa  na biashara zingine , hizo zinaweza kabisa kunifanya niendelee kuishi pale nitakapochukua huo uamuzi.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.