“Siamini kama bff anaweza kunifanyia vitendo vibaya”-Wolper

Msanii wa Bongo Movies na mjasiriamali ambae amekuwa na skendo za hapa na pale mitandaoni lakini amekuwa akionesha kuzoea na kutokujali maneno ya watu Jackline Wolper   ameongea na kufunguka kuwa mpenzi wake mpya aliyenae sasa hivi ambae pia ni   mwanamitindo   anaejulikana kwa jina la Brown ambae yeye  Wolper amezoea kumuita ‘bff’ kuwa mwanaume huyo  ndie mwanaume anaemuamini sana na anajua kuwa ni mwanaume wa tofauti kuliko wanaume aliowapitia hapo awali.

Wolper ambae alikuwa katika mahusiano ya kimapenzi  na msanii wa muziki wa Bongo Fleva Harmonize na kuachana hivi karibuni kwa kutupiana maneno katika mitandao  alimsifia mpenzi wake huyo mpya na kusema kuwa kaka huyo ni mcha Mungu sana hivyo anaamini hawezi kufanya mambo mabaya kabisa kama kule alipotoka.

download latest music    

Ingawa wolper ameonekana kukiri kuwa katika mapenzi wanaume sio wa kuwaamini na wengi wana matendo ya kufanana, lakini anaamini bff wake hawezi kufanya mambo kama hayo.

“Siamini kama bff anaweza kunifanyia vitendo vibaya kama nilivyowahi kufanyiwa  hapo awali .Namuamini sana kutokana na kuwa yeye   ana hofu ya Mungu , lakini sisi bado ni binadamu,anaweza kunikosea kawaida au mimi nikamkosea hiyo ni kawaida  kwa sababu sis ni binadamu  hiyo haitanifanya nimchukie, lakini akifika huku pa kunifanya  niumie kama nilikotoka nitaamini kuwa hakuna wa kumuaini tena katika mapenzi ” anasema Wolper.

Licha ya bifu zinazoendelea kati yake yeye na mpenzi wake wa zamani  na kuumizwa na mwanaaume huyo kama anavyodai yeye mwenyewe lakini bado  anaamini kabisa kuwa mwanaume aliyenae sasa ndie mwanaume aliyekuwa anamtaka na kumtafuta siku zote sababu ni mcha Mungu na ana heshima pia.

Ingawa kumekuwa na maneno mengi  katika mitandao watu wakisema  tangu awe na mahusiano  na  mwanaume huyo aliyenae sasa kuwa ni mdogo huku watu wakimuita Wolper ‘sugar mamy’, lakini kwake hajali maana anaamini kuwepo kwa mapenzi ya kweli kati yake na bff , hivyo kwa Wolper umri sio kigezo cha kumtenganisha na bff wake

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.