Sijaangalia Video Naogopa, Nitaangalia Nikitulia:-Martin

Aliyewahi kuwa meneja wa mwanadada wema sepetu martin kadinda amefunguka na kusema kuwa kwa kitendo cha wema kuomba msamaha kinaweza kuwa ni jambo kubwa ambalo wema amejifunza na kujutia kile alichokifanya.

Martin anasema kuwa kuna mambo mengi ya wema machafu yamewahi kutokea lakini hajawahi kuita waandishi kwaio kwa hili linaweza kuwa kubwa litakalo weza kumrekebisha sana na kuanzi sasa anaamini kuwa  ataanza kubadilika.

download latest music    

ninaamin kuwa kila mtu ana makosa hata wewe  uliyepo nje ya kamera pia una makosa, na ili uweze kujifunza na kukua lazima kuna mahali unaweza kukosea na kuweza kurekebishwa.kwaio  kitendo cha kuita waandishi ni kitendo cha kuonyesha kuwa kweli amekosea na anataka kujifunza, aliniambia kuwa anahitaji press nyumbani kwa mama yangu nikajua ni muda muafaka wa yeye kuongea na watu wake.

kwa sababu sasa hivi ameweza mpaka kuita press basi ni kweli atakuwa amejifunza, video sijaina ingawa ipo kwenye simu yangu lakini sijataka kuifungua kwa sababu ujumbe tu unaogopesha.nina shughuli kubwa ya kufanya ijumaa nikitulia na kumaliza shughuli zangu nitaiangalia.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.