Loading...

“Sijaona Hasara Kufungiwa Bongo Bahati Mbaya”- Young Dee

March 07, 2018 at 05:39
“Sijaona Hasara Kufungiwa Bongo Bahati Mbaya”- Young Dee

Mwanamuziki wa Bongo fleva Young Dar es salaam, Young D amefunguka na kudai hajaona kama amepata hasara yoyote kwa ngoma yake ya Bongo bahati mbaya kufungiwa.

Wiki iliyopita TCRA walitangaza rasmi kuwa wamefungia nyimbo 15 zisipigwe kwenye vyombo vya habari kwa kile walichodai kuwa BASATA wamezipitia na kuagiza zifungiwe kwa kukosa maadili ya Kitanzania.

download latest music    

Moja kati ya wasanii waliofungiwa ni Young Dee ambapo wimbo wake uliofungiwa unaitwa Bongo Bahati Mbaya (BBM) kwenye wimbo huo Young Dee anaimba kuwa hajapenda kuzaliwa Tanzania bora angezaliwa mbele pia wimbo huu ulikosolewa na Waziri Mwakyembe.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo Tv, Young Dee amefunguka na kusema Kufungiwa kwa wimbo wake wa Bongo Bahati Mbaya ilikuwa ni Ghafla na hakupewa taarifa yoyote hapo kabla wala kuonywa zaidi ya kuona kwenye mitandao ya kijamii lakini pia amekiri kuwa mpaka hivi sasa hajaona sababu ya wimbo huo kufungiwa Nay haelewi wanataka nini na nini hawataki.

Young Dee amesisitiza kuwa mpaka hivi sasa hajafikiria kwenda BASATA kuulizia kuhusu wimbo wake kufungiwa kwani mpaka hivi sasa hajaona hasara ya nyimbo hiyo kufungiwa labda atakuja kuiona mbeleni lakini hivi sasa.

Loading…

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment