“Sijawahi Kushuka Kwenye Muziki”-Queen Darleen

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB, Queen Darleen ameibuka na kudai kuwa yeye ni msanii wa kike ambaye hajawahi kushuka Kwenye chati.

Queen Darleen ambaye hivi sasa amesainiwa chini ya Label ya kaka yake Diamond Platnumz, WCB amedai pamoja na kwamba ni mkongwe lakini hajawahi kushuka na mpaka sasa anakimbiza na wasanii wapya kama Nandy na wengineo.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Wasafi TV, Queen Darleen amesema kuwa yeye hajawahi kushuka toka enzi hizo na kujifananisha na marehemu Bi. Kidude kuwa mzee wake utaendelea kuwa mzuri hata umri wake ukiendelea kumtupa mkono.

Mimi sijui wao lakini mimi toka  hizo zama za kina Lady Jaydee, akina Ray C mpaka leo hii mimi bado nipo, nakwenda nao level za akina Nandy, yaani mimi nipo humo humo na sitoki yaani na wasitegee kutoka leo, kesho yaani mimi kama bi Kidude nakufa na muziki wangu”.

Lakini pia Darleen amewatolea povu zito mashabiki ambao wamekuwa wakiponda mavazi yake anayovaa:

Kama mimi navaa najiona mwenyewe napendeza, niko fresh, lakini mtu anakuja anakwambia unavyovaa umevaa vibaya hujapendeza? My Friend pesa yangu ambayo nimenunulia nguo mimi unayoniambia sijapendeza, hiyo simu yako uliyoshika gharama yake hazilingani.. Tusipangiane mavazi wala maisha”.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.