Sijawahi Kutunga Wimbo Kumchamba Mtu :-Isha mashauzi

Msanii wa taarabu nchi  ISHA MASHAUZI amefunguka na kukanusha kuwa amekuwa aktunga nyimbo kwa ajili ya kuwa-attack wasanii wengine ikiwa kama njia ya kugombana nao na kuepuka kuwafata moja ka moja.Isha anasema kuwa yeye ndio amekuwa akitunga mashairi ya nyimbo zake lakini hajawahi kufanya hivyo kwa ajili ya kumsema au kumchamba mtu vibaya.

Isha anasema kuwa kamwe haweiz kufanya hivyo na kama kunamwatu wanakaa na kujaribu kutunga nyimbo ambazo zinakuwa ni kama majibu ya nyimbo zake basi anakuwa akijisumbua kwa sababu yeye hashindai na mtu na kama kuna mtu anakaa akifanya hivyo anakuwa akijisumbua tu.

download latest music    

Akijaribu pia kuwajibu wanaomsema vibaya hasa baada ya kuvaa suruali katika nyimbo zake, anasema kuwa kwa kawaida msanii ni lazima kubadilika badilika hivyo yeye haoni kama anakosea kufanya hivyo kwa sababu yeye ni msanii.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.