Siku Moja Baada ya Mazishi, Baba Aondoka na Mtoto Wake

Ikiwa imepita siku moja mabpo mazishi ya mwanadada Agness Masogange yamefanyika siku ya jumatatu tarehe 23 April, baba wa marehemu amethibitisha kuwa mjukuu wake Sania ambae ni mtoto wa marehemu ameondoka na baba yake kwenda jijini Dar Es Salaam siku iliyofuata.

Akiongea na waandishi wa  habari, baba wa marehemu Mzee Gerald waya ansema kuwa hakuwahi kumjua baba wa mjukuu wake mpaka msiba huu ulipowakutanisha lakini kwa kuwa hakuna shughuli yoyote ya kifamilia inayoendelea , mjukuu wake ameondoka kurudi dar kutokana na swala la masomo.

download latest music    

mjukuu wangu sanii ameondoka  leo alfajiri na baba yake kwa sababu tumeona hakuna shughuli zozote za kifamilia zote ziliisha jana , ni bora aende kuwahi masomo.Watakuja hapa tena wakati wa kumalzia matanga.

Mzee Waya anasema kuwa shughuki za matanga zitafanyika baada ya siku 40 baada ya msiba na zitafanyika nyumbani kwenye asili ya ukoo wao ambapo pia kuna kaburi la agness ili kumaliza msiba lakini kwa siku ya jana walifanya shughuli yashughuli za kwaaga waombelezaji ili wanaorudi jijini waweze kurudi salama na hapo nyumbani wamebaki ndugu tu.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.