Sikuwahi Kuwaza Kuwa Single Mother:-Faiza Ally

Msanii wa Maigizo nchini faiza ally amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake ya ukuaji hakuwahi kuwaza kuwa single mother hata siku moja .Faiza anasema kuwa hata baada ya kupata mtoto alikuwa akijiuliza sana ni kwa sababu ya mwanaume ndio maana anaishi maisha ya kuteseka.

Katika Ukurasa wake wa Instagram Faiza Ally aliandika kuwa amekuwa katika wakati mgumu sana kuwa single mom lakini bado anajifariji kuwa ni bora kuliko mke.

download latest music    

Wakati nakua sikuwahi kuwaza kuwa single mom, lkn kutokana na misimimo yangu wanaume wajinga hawakunielewa nikajikita ktk kujitegemea, baada kuwa mama nikawa najiuliza ni kwa sababu tu ya mwanaume au baba mtoto ndio niishi maisha nisiyo yataka , nikaondoka nikiwa nauchungu mwingi mno lkn nikasema maisha yangu ni bora kuliko kuwa mke! Nikapitia mengi sana haikua rahisi lkn Leo nimesimama imara kwa sababu niliamua kuchagua maisha ninayo ishi kwa hiari ! Nilipita wapi na nikavuka vikwazo vyote ????? Njoo nita share stori yangu na wewe kuwa single mom sio mwisho wako ! Kuna maisha zaidi ya kukaa usipo stahili ! JUA THAMANI YA UANAMKE WAKO BILA KUJALI WANAO BWEKA NJIANI“.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.