Sina Bifu na Snura Ila Sio Rafiki Yangu- Nisha

Muigizaji wa Bongo movie Nisha aliyetoa nyimbo yake mpya ‘Bachela’ amefunguka kuhusu uhusiano wake na msanii wa Bongo fleva Snura na kusema hana bifu naye ila pia sio marafiki.

Ishu ya Snura na Nisha ilishika headlines sana wiki chache zilizopita baada ya Snura kuonekana ana uhusiano wa kimapenzi na Minu Calypto ambaye alikuwa ni mpenzi wa Nisha.

download latest music    

Taarifa zilienea na kudai kuwa Snura alimpindua NIsha kwa Minu ambaye alikuwa ni kiben 10 cha Nisha na hata maneno maneno yalisemwa Kwenye mitandao ya kijamii ingawa kila mmoja alisisitiza kuwa hana bifu na mwenzake.

Kwenye mahojiano aliyofanya hivi karibuni na Millard Ayo Tv, Nisha ameweka wazi kuwa hana bifu na Snura wala hawana urafiki ila ni watu tu ambao wanafanya wote sanaa zao:

Mimi na Snura hatuna urafiki ni wasanii tu lakini pia hatuna Uhasama wowote wala bifu kwa sababu mwisho wa siku maisha yanaendelea kwa sababu aliyekuwa naye nilishaahana naye kabla hata hawajaanza mahusiano kwaiyo moyo wangu mweupe kwake”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.