Sina Mpango wa Kuolewa-Lady JD

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Judith Wambura maarufu kama Lady Jay Dee amefunguka na kusema watu wasitarajie kuona ndoa yake hivi karibuni maana hana mpango wa kuolewa.

Lady JD alifunguka hayo alipokuwa anamuongelea mpenzi wake msanii kutoka Nigeria anayejulikana kama Spicy Music, baada ya kutomposti Kwenye ukurasa wake wa Instagram tangu Tarehe 4 April.

download latest music    

Lady JD ameweka wazi kuwa yeye na Spicy Music hawajaachana kisa tu hamposti Kwenye page yake ya Instagram bali hajaona sababu ya kumuweka humo kwani kipindi anamposti sana ilikuwa ni kwa sababu ya kazi ya wimbo wao pamoja.

Lakini Kwenye mahojiano yake na Bongo 5 Lady Jay Dee ameweka wazi kuwa pamoja na kwamba yupo Kwenye Mahusiano lakini watu wasitegemee kumuona anaolewa anytime soon:

Watu wasitarajie kuona ndoa yangu anytime soon wasisahau kuwa sio kwamba mimi sijawahi kuolewa, au kuwa nataka sana kuolewa. Kuolewa ni jambo la kujipanga na kwa sasa siko tayari kuolewa na mtu yoyote naweza kuwa na Mahusiano na mtu lakini siko tayari kwa ndoa! Sio sasa”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.