“Sio Kiki Mimi na Ben Pol ni Wapenzi”- Ebitoke

Mchekeshaji kutoka Timamu tv asiyeisha vituko, Ebitoke amefunguka na kusisitiza kuwa yeye na staa wa Bongo fleva Ben Pol wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi na sio kiki kama wengi wanavyosema.

Tangu walivyotangaza kuwa wapo kwenye mahusiano Kumekuwa na tetesi nyingi huku watu wengi wakidai kuwa hawana mahusiano yoyote bali wanatafuta tu kiki ili Ben Pol auze mziki wake na Ebitoke ajulikane kwa komedi.

download latest music    

Lakini mara kwa mara Ebitoke amekuwa akisisitiza kuwa wenyewe wapo kwenye mahusiano na amekuwa akisisitiza kuwa anampenda sana Ben Pol ingawa inasemekana ana mpenzi mwingine.

Ebitoke ameendelea kukiri penzi lake na Ben Pol Kwenye interview aliyofanya na Bongo 5 ambapo amedai kuwa hawatafuti kiki bali wapo kwenye penzi zito:

Watu wengi wanajua mimi na yeye hatuna mahusiano na watu wameshakariri kama ni kiki ila tumewaacha waendelee kuwa na mtazamo huo wanaouona lakini mimi na Ben Pol tunaendeleza mahusiano yetu na tunafnya kimya kimya. Ben Pol amefikia hatua ya kunisapoti na mimi huwa namsapoti maana huwa tunasapotiana kwaiyo mkiwa pamoja lazima mambo yawe hivyo”.

Lakini pia Ebitoke amefungukia tetesi zinazomzunguka mchekeshaji mwenzake Mama Ashura ambapo inadaiwa Ebitoke alimuibia bwana, jambo ambalo amelikataa na kusema kuwa Mama Ashura yupo anatengeneza kazi zaidi siku si nyingi ataonekana.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.