Siri ya Mahusiano ya Mzungu na Nisha Yafichuka.

Hivi karibuni mwanadada Nisha alikuwa akiweka picha na video katika ukurasa wake wa instagram na hata alipohojiwa alisema kuwa kwa sasa ameamua kutoka katika mahusiano na vijana weusi na kuamua kuingia katika mahusiano na wazungu akiamini kuwa hao watakuwa na mapenzi ya kweli na sio vinginevyo.

Lakini baada ya muda mfupi ilitoka video ilimuonyesha nisha ambae kwa sasa ameamua kujiingiza katika sanaa  ya muziki akiwa  na mzungu huyo kama video model wake.lakini hiyo haitoshi kusema kuwa waili hao sio wapenzi hivyo baadhi ya magazeti yaudaku yakianza kufukunyua kuhsusu undani wa mzungu huyo.

download latest music    

Kwa bahati nzuri alipatikana mwanamke wa mzungu huyo ambae hapo awali alilalamika kuibiwa mume wake lakini sasa hivi anaonekana yupo sawa baada ya kupata ufafanuzi wa kile alichokuwa akikifanya mume wake.

Mwanadada huyo aliejitambulisha kwa jina la Felister anasema kuwa nisha alikuja nyumbani kwao na kumuomba mme wake ili waende kushoot video ambapo hata zile picha zilikuwa zipo katika huo wmbo lakini haikuwa makubaliano yao kuwa akatangaze kuwa yuke ndio mwanaume wake.

Kwa kumalizia mwanadada huyo alisema kuwa kwa sasa walishaongea na wameyamaliza na kila kitu kipo sawa.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.