Sista Fey Amtolea Uvivu Steve Nyerere

Msanii wa Bongo movie Faidha Omary maarufu kama Sista Fey amemjia juu msanii mwenzake Steve Nyerere na kumuita mnafiki huku akimtuhumu kwa kusababisha mpaka yeye kukamatwa na kuwekwa ndani.

Sista Fey alikamatwa wiki chache zilizopita kutokana na kudaiwa kuanika maudhui mabaya kwenye mitandao ya kijamii lakini hivi sasa ameibuka na kumnyooshea kidole Steve Nyerere kama mtu aliyesababisha hayo yote.

download latest music    

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari, Sista Fey alimwaga povu hili;

Hapa Tanzania hakuna msanii mnafiki kama Steve Nyerere kwani anakusema asubuhi jioni anajifanya rafiki yako ila namuombe kwa Mungu aendelee na unafiki wake na hivyo anavyojifanya mwema kumbe mnafiki tu”.

Steve anajifanya kimbele mbele zaidi ya viongozi wetu halafu mimi kama Fey najua hakuna nilichokukosea ila roho yako mbaya uliyotengeneza kwanini mimi nionekane sana Instagram kuliko wewe itakugharimu kwani kila mwanaadamu ana karama yake wewe karama yako kuiga sauti za viongozi wewe sio kiongozi”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.