Sister Fey Amfungukia Mazito Hamisa Mobetto

Msanii wa Bongo fleva Faidha Omary maarufu kwenye mitandao ya kijamii Kama Sister Fey ameibuka na kumpa maneno mazito Mwanamitindo Hamisa Mobetto.

Sister Fey amemuibukia Hamisa na Kumpongeza kwa mambo mazuri anayofanya hivi sasa nchini Marekani ambapo anafanya shoo mbali mbali katika nini mbali mbali.

download latest music    

Sista Fey amemtaka kuwa jasiri na kutoangalia nyuma sasa kwani alipotoka ni mbali lakini alipofika hivi sasa ni mbali zaidi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Sista Fey ameandika maneno haya:

Uanawza ukatukanwa Sana na ukadhalilishwa sana ukapitia magunu mpaka ukajiuliza kwanini Mimi? ILA siku ni moja tu kila mmoja atashangaa hata maadui zako watajificha kukuangalia kimya kimya wakati wa Mungu ni wakati sahihi but Hamisa nakuomba na kukuombea usirudi nyuma ikiwezekana kweli chukua uraia huko na ikishindikana piga kazi haswa hakikisha unapata madili mengi ili uzidi kuwanyamazisha wabaya wako Misa dunia dura mama na sitamani kusikia utoto umekurudisha nyuma kwa uliyopitia jione una miaka 40 wewe ni mrembo”.

 

Hamisa tangu ameachana na Diamond na kuelekeza nguvu zake kwenye kupiga kazi ameonekana kufanya vizuri na kufika mbali zaidi.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.