Sister Fey Aomba Msaada

Mwanamuziki wa kike nchini asiekosa drama kila kukicha katika mitandao ya kijamii ametuma video katika ukurasa wake wa instagram akiomba msaada kwa mshabiki na watanzania kwa ujumla baada ya kuachana na mume wake.

Sister Fey anasema kuwa anajua ameshafanya mambo mengi ambayo yamekuwa yakimdhalilisha lakini anaomba msamaha na kuacha kumsakama na kuangalia ya mbele na kumsaidia kwa shida aliyoileta mbele ya mashabiki zake.

download latest music    

Sister Fey anasema kuwa anaomba sana kupata pesa kwa ajili ya kulipa kodi ya nyumba kwa sababu endapo hatopata pesa hiyo basi anaweza kufukuzwa katika nyumba anayokaa kwa sasa na hatojua wapi atakimbilia kwa sasa.

Ikumbukwe kuwa siku chake zilizopita, mwanadada sister Fey alitangazwa kusaini mkataba  wa kampuni mpya nchi kenya kwa ajili ya kusimamia kazi zake.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.