Sitaacha Kuwakomesha Wanawake Wenzangu- Jacqueline Wolper

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabishara maarufu  Jacqueline Wolper amefunguka na kudai kuwa hatoacha kuwakomesha na kuwasema wanawaje wenzake wote ambao hawataki kujishughulisha.

Wolper ambaye mbali na kufanya vizuri katika tasnia hii ya sanaa ya Bongo movie bali amejikita ni moja kati ya wafanyabiashara wazuri kwani ana duka lake la nguo/ boutique ambalo anashona na kuuza nguo linaloitwa ‘Wolperstylish’.

download latest music    

Wolper amefunguka na kusema kuwa kamwe hataacha kuwakomoa na kuwasema wanawake wenzake ambao wameishia kujibweteka tu majumbani na hawataki kujishughulisha kwa jambo lolote wala jambo lolote.

Wolper amefunguka hayo kwenye interview yake aliyofanya na Friday Night Live ya East Africa TV ambapo amesema kuwa ni wakati sasa wa mabinti kuacha kutegemea pesa wanazopewa na wanaume na badala yake wajishughulishe ili kutengeneza pesa zao wenyewe:

Nataka niongee na wadogo zangu wa kike 2018 mimi naendelea kuwatia hasira na kuwaambia kuwa hela ya mwanaume sio yako, ukishachukia pesa ya mwanaume Fanya kitu chako ili iwe yako usikubali kunyanyasika kwa pesa za mtu mwingine, kwaiyo wadogo zangu wanawake wenzangu nitaendelea Kuwa inspire ili ufanye kazi ili utambue hela yako, kamwe usitambue hela ya kuhongwa kama yako”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.