“Siwezi Kuachika Kirahisi “- Shamsa Ford

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford ameibuka na kudai kuwa hawezi kiachika na Mume Wake Chiddi Mapenzi kirahisi kama watu wengi wanavyofikiri.

Shamsa amefunguka na kusema kuwa anawashangaa wanaomtolea maneno ya kwamba ameachika kila anapoposti chochote kwenye mitandao ya kijamii.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Dimba, Shamsa alisema kuwa wanaosubiri ndoa yake ivunjike watasubiri sana, kwani yeye ni mwanamke anayejiamini na kutambua thamani ya mume wake.

Kila nikiposti kitu watu wanahusisha na mimi kuwa kwenye mgogoro na mume wangu Chid Mapenzi, nipende kuwaambia tu hakuna kitu kama hicho, bado tunapendana sana na tuna mikakati mingi ya kuhakikisha hakuna linalotuyumbisha”.

Shamsa amesema hayo kutokana na tetesi zilizosambaa kwenye Mitandao ya kijamii kuwa ameachana na mume Wake Chiddi Mapenzi kutokana na kuposti maneno yenye utata kuashiria Ndoa Yake kuvunjika.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.