“Siwezi Kumsaliti Ochu” -Witness Kibonge Mwepesi

Msanii wa Bongo Fleva  mkongwe,alieanza musiki miaka mingi iliyopita lakini mpaka sasa bado anawika katika nyanja hizo, ambae pia ni  Rapper wa kike anaetumia mwili wake vizuri na haujawahi kumshinda katika kazi zake  Witness Kibonge Mwepesi  amemsifia mpenzi wake  na baba mzazi wa mtoto wake lakini msanii mwenzie pia OchuSheggy na kusema kuwa anampenda sana kuliko kitu chochote na hata kaa amsaliti hata siku moja.Katika ukurasa wake wa instagram Witness aliandiaka sifa hizo nyingi  kwa  baba mzazi wa mtoto wake huyo kuwa ni mwanaume wa tofauti kuliko watu wanavyodhani , anasema kuwa kwa upande wake hawezi kumsaliti mwanaume huyo labda yeye aanze kuzingua.

“Ninampenda huyu mwanaume, tofauti na mnavyodhani, na siwezi kumsaliti na mtu awae yeyote yule , labda azingue yeye kwa mengine ila kwangu mimi siwezi liharibu penzi letu”ameandika Witness

download latest music    

Witness na OchuSheggy wamekuwa katika mahusiano kwa muda wa miakaa  zaidi ya mitano sasa na wamebahatika kupata mtoto mmoja , yeye na  mumewe na wamekuwa wakisapotiana katika kazi zao za kimuziki na kuna baadhi ya nyimbo wamekuwa wakiimba pamoja mfano wimbo wa Sharifa  “penzi letu linaelekea miaka mitano sasa toka tuwe pamoja na lipo kama ndio kwanza tunatongozana “aliongezea Witness

Witness ameelezea pia sababu inka,ayoyawafanya wawili hao waendelee kupendana na kudumu katika mahusiano yao ya kimapenzi “kilichopo hapa ni chemistry inayotengeneza utulivu wa moyo na si chemicals za kuharibu afya na amani ya moyo!”anaongea  Witness.

Wawili hawa wamekuwa moja ya wapenzi wa kuigwa kwa sababu wamekuwa katika mahusiano kwa muda mrefu huku wote wakiwa ni wasanii lakini imekuwa tofauti  kwa mahusiano ya wasanii wa kitanzania ambao mahusiano yao hayawezi kukaa kwa muda mrefu bila kuachana . mahusiano ya wawili hao yamedumu kwa muda mrefu na wanaonekana kujiheshimu na kupendana kama anavyodhiirisha witness mwenyewe.

Witness anaejulikana kwa nyimbO zake kama Mzuka, Jirani aliyomshirikisha Snura na Mzee Yusuph, Buku jero na nyingine nyingi anaweza kuwa  mfano wa kuigwa kwa wasanii wa kike.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.