Loading...

“Siwezi Kurudiana na Mkongo Tena”- Wolper

December 17, 2018 at 06:45
“Siwezi Kurudiana na Mkongo Tena”- Wolper

Muigizaji wa Bongo movie na Mbunifu wa mavazi Jacqueline Wolper amefunguka na kuweka wazi kuwa hawezi tena kurudiana na aliyekuwa Mpenzi Wake anayejulikana Kama Putin maarufu kama Mkongo.

Tetesi za Wolper kurudiana na aliyekuwa mchumba Wake zilisambaa Wiki iliyopita Kupitia mitandao ya kijamii Baada ya Wolper kumposti katika ukurasa Wake wa Instagram.

Loading...

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Wolper alisema kuna watu wamekuwa wakivumisha kwamba amerudisha mapenzi kwa Mkongo huyo kwa sababu tu wanapostiana picha kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram, lakini hiyo siyo sababu ya kurudisha penzi lao la nyuma bali wanafanya hivyo kimazoea tu.

Watu wanaonijua vizuri wanafahamu, siwezi kurudia matapishi yangu hata siku moja. Huyo Putin tumekuwa kama washikaji tuliozoeana, lakini hakuna mapenzi tena na hatuwezi kuwa wapenzi tena”.

Wolper na Putin walikuwa kwenye mahusiano kwa muda mwaka mmoja ambapo walifikia hatua ya kuvalishana pete ya uchumba, lakini waliachana baada ya mwanaume huyo kugundulika kuwa ana mwanamke mwingine nchini kwao.

Share

Comments

  1. matapishi tena…

  2. kwani Wolper na urembo wake wote hawezi akapata mwanamume mwengine mpya ni kurudiana na ma ex tu

  3. yataka galby

  4. wolper nakupenda mpaka naumwa yaani. Usiwasikize mahaters hawakosi la kusema

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…