“Siwezi kutoa nyimbo mpya kila siku”-Lady Jay Dee

September 13, 2017 at 11:12
"Siwezi kutoa nyimbo mpya kila siku"-Lady Jay Dee

Msanii  mkongwe kabisa wa kike kutoka tanzania ambae alianza muziki na bado  anaendelea nao kwa mud amrefu pamoja na kuwa game linazidi kubadilika lakini bado yuko imara katika kazi zake mwanadada jay dee  amefunguka na kusema kuwa hawezi kuwa anatoa nyimbo mpya  kila siku kwa sababu anaamini kuwa nyimbo zake ni nyimbo zenye hisia sana na huishi muda mrefu hivyo si lazima kutoa nyimbo nyingi kwa wakati mmoja.

Mwana dada huyo ambae hivi juzi ametoa wimbo mpya unaokwenda na jina la ‘i miss you’ ambao umetengenezwa na producer man water ambae pia ametengeneza nyimbo zake nyingine nyingi ikiwepo ule wa ndindindi  anasema kwa sasa wasanii wengi wamekuwa wakitoa nyimbo mfululizo  bila kujali kuwa wimbo uliopita umekaa kwa muda gani,”siwezi kuwa natoa nyimbo mpya kila siku ,kwa sababu nyimbo zangu ni za hisia sana ambazo zinaweza kukaa hata  miaka kumi.Ni bora nitoe wimbo mmoja  kwa mwaka  lakini uwe  unaishi miaka mingi kwa  ladha ile ile  siku zote‘  amesema jay dee

Akizungumza na kipindi cha planet bongo cha East Africa Radio ,pia lady jay dee amepata nafasi ya kuzungumziz kwa ufupi hali ya usalama inayoendelea nchi ikiwepo kuuawa na kutekwa kwa baadhi ya watu maarufu akiwepo msanii wenzio roma mkatoliki lady jay dee anasema “kitendo cha mtu kuweza kupigwa risasi  hadharani inatishia amani sana, vilevile kuna wasanii walikuwa wametekwa,unaogopa,sehemu yenye amani vitu kama hivi haviwezi kutokea,ninaweza nisiwe na maneno ya kusema nikabaki kusikitika tu kwasababu sio mambo mazuri haya yanayotokea,na yanaonyesha kuwa sio kuzuri tunakoelekea”  ameongezea dada mkubwa.

Lady jay dee ni moja  kati ya wasanii wakongwe kabisa wenye mchango mkubwa katika kukuza sekta ya muziki wa bongo fleva Tanzania na amekaa katika kazi hii zaidi ya miaka kumi na bado nyimbo zake zimekuwa ni nyimbo zenye kupendwa na mashabiki sana ,kiasi kwamba hata zile  za zamani bado zinapendwa na watu .

 

Leave a Reply

7 Comments on "“Siwezi kutoa nyimbo mpya kila siku”-Lady Jay Dee"

avatar
Sort by:   newest | oldest | most voted
Abdul Fauda
Guest
Abdul Fauda

nyimbo zako ni motoooooooooooooooo

Habiba
Guest
Habiba

uko makini sana jide

Happiness Diana
Guest
Happiness Diana

Jide mashinee

Godbless Mwanga
Guest
Godbless Mwanga

Mwenye mziki wake

Jessica Michael
Guest
Jessica Michael

Nakuelewaga sana mdada wewe

Neema Kagera
Guest
Neema Kagera

Hapo umenena ukweli,hawa WCB kila siku wanatoa maana nyimbo zao mashuzi sana

MC Mambo
Guest
MC Mambo

LJD umenena sawa! Nyimbo utitiri si issue…angalia mfano wa ule wimbo “Malaika….Nakupenda Malaika…!” una miaka mingi na unapeta!


in Entertainment
Loading...
wavatar

#Godseeker,
I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.

error: Content is protected !!
error: Content is protected !!