Snura Afungukia Kupora Bwana wa Nisha, Akubali Kuwa ni Mpenzi Wake.

Mwandada naesifika kwa kutoa mauno anapokuwa jukwaani snura majanga amefunguka na kukubali kuwa ni kweli mwanaume yule ambae picha zake zimevuja ni mpenzi wake lakini sio kweli kuwa mwanaume huyo amempra kutoka kwa nisha kama tetsi na taarifa zinazokuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii.

Snura ambae kwa muda mrefu alikuwa akikana kuwa hana mahusiano na mwanaume huyo , aliumbuka sana siku ya wapendanao baada ya baadhi ya watu kudaka picha zake zikimuonyesha yuko na mwanaume ambae watu walikuwa wakimtuhumu kuwa amempora kutoka kwa msanii mwenzake Nisha ambae pia kwa muda mrefu amekuwa akilia kuwa amekuwa akiibiwa mabwana kila kukicha.

download latest music    

Baada ya kuvuja kwa picha hizo Snura aliona ni bora kuweka bayana swala hilo kwa sababu amekuwa akiandamwa na kukosa amani ya kuwa na mwanaume huyo kwa sababu ya kusimangwa na marafiki na mashabiki zake katika mitandao.

Nisha alikubalikuwa ni kweli wapo katika mapenzi mazito na mwanaume huyo lakini sio kweli kuwa amemuiba mwanaume huyo bali mwanaume huyo aliingia nae katika mahusiano tayari alikuwa amekwisha achana na Nisha siku nyingi na ukweli ni kwamba ni nisha mwenyewe ndie aliwaunganisha wawili hao kwa sababu ya kufanya kazi pamoja.

Minihai sio mpezni wa nisha na hata sikumchukua kwake,kwani hadi naningia katika mahusiano na mwanaume huyo tayari alikuwa maeshaachana na Nisha siku nyingi na hata aliyetunganisha ni yeye mwenyewe Nisha kwa sababu alimpa Minihali namba yangu ya simu.

Snura alisema kuwa amekuwa akiwashanga watu ambao wanamsema katika mitandoa kwa kumtuhumu kuwa ameiba mwanaume wa nisha wakati ukweli ni kwamba aliyewaunganisha ni nisha mwenyewe na hata kuingia katika mapenzi iliwachukua muda mrefu kwa sababu walikuwa wakifanya kazi kwa pamoja na kujikuta wanazoea sana na kuingia katika mahusiano.

Siku za nyuma baada ya kuanza kwa tetesi hizo, msanii Snura aliwatolea povu zito kipindi cha shilawadu kwa kusambaza taarifa za uongo kuhusu mahusiano hayo lakini baada ya picha za Snura na mwanaume huyo kuvuja imemfanua Snura kufunguka na kusema ukweli.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.