Snura Azungumzia Bifu lake na Shiloleh

Msanii wa muziki wa Bongo fleva, Snura Mushi ‘Snura’ amefunguka kuwa uhusiano wake na msanii mwenzake Shilole haujawahi kubadilika tangu mwanzo na hawakuwahi kuwa na tofauti kama wengi wanavyodai.

Snura amefunguka hayo wakati akizungumza na www.eatv.tv, ambapo amesema kuwa Shilole na yeye walikuwa na mpango wa kufanya kazi wakati ule ili kuonesha kuwa hawakuwa na tofauti lakini muda ulikosekana.

download latest music    

“Uhusiano wangu na Shilole haujawahi badilika, upo vilevile tangu tulipozaliwa na umesimama palepale kama picha la ‘bisimini'”, amesema Snura.

Akizungumzia mafanikio yake katika sanaa, Snura amesema kuwa anajivunia vitu vingi ambavyo amevipata kupitia muziki lakini hapendi kuonesha.

Nina vitu vingi vya kujivunia lakini siwezi kunadi mali zangu mtandaoni, mimi huwa na nadi kazi tu”, amesema Snura

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.