Snura: Bado Sijajua BASATA Wanataka Kitu Gani

Mwanamuziki wa Bongo fleva Snura makali wa ‘Majanga’ amefunguka na kusema kuwa anawashangaa sana BASATA kwani mpaka sahivi hajajua wanataka nini au wanaangalia vigezo gani.

Wiki iliyopita TCRA walitangaza rasmi kuwa wamefungia nyimbo 15 zisipigwe kwenye vyombo vya habari kwa kile walichodai kuwa BASATA wamezipitia na kuagiza zifungiwe kwa kukiuka desturi na  maadili ya Kitanzania.

download latest music    

Snura ni moja kati ya wasanii waliofungiwa nyimbo mbili ambazo ni ‘Nimevurugwa’ na ‘Chura’  ambao ulizua gumzo tangu ulipokuwa unatoka mwanzoni kabisa ambapo ilidaiwa kuwa hauendani na maadili ya Kitanzania.

Snura amefanya Interview na Millard Ayo Tv lakini ameonyeshwa kushangazwa kuliko hata kukasirika kutokana na kitendo hiko ambapo amefunguka na kusema:

Kabla ya hapo sikupata taarifa yoyote kuwa nafungiwa nyimbo zangu kwa sababu wakati nafungiwa Chura nilitumiwa barua lakini safari hii sikuitwa wala sikuwa na taarifa yoyote ile kwaiyo kwa hilo nakuwa nashindwa kuwaelewa BASATA wanakuwa wanataka nini kutoka kwangu”.

Snura amedai alishawahi Kuitwa na BASATA ambapo walifanya kikao na kuamua kuwa video ya wimbo wa Chura ndio ulikuwa mbaya lakini audio ilikuwa nzuri hivyo aliambiwa abadilishe video na hatafungiwa nyimbo hiyo ambapo amedai alifanya video mpya ambayo waliikubali na kuipitisha.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.