Loading...

Snura- Natamani Ningepata Nafasi Ya Kusoma Zaidi

March 13, 2018 at 08:18
Snura- Natamani Ningepata Nafasi Ya Kusoma Zaidi

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya mduara Snura Mushi ‘Snu sexy’ amefunguka na kusema majuto yake maisha ni ni kukosa elimu.

Snura ambaye amekiri kuwa aliishia elimu ya msingi na hakufanikiwa kabisa kukanyaga elimu ya sekondari kutokana na maisha kuwa magumu na wazazi wake kukosa uwezo wa kumsomesha na kumfikisha mbali kielimu.

Loading...

Snura amelifungukia gazeti la Ijumaa Wikienda na kueleza jinsi anavyojikuta akizitolea macho sare za shule za sekondari kwani hakubahatika juzi ana kabisa:

Kiukweli nikaona wasichana wamevaa sare za sekondari huwa nazitolea macho sana natamani siku zirudi nyuma ili nami nipate elimu hiyo kwani maskini niliishia darasa la saba tu”.

Snura pia ametoa ushauri kwa wasichana ambao wamepata nafasi ya kusoma watumie nafasi hiyo kusoma kwa bidii na kuachana na mambo ambayo hayana faida kwani mtu kama yeye hakubahatika kabisa kupata nafasi hiyo ya kuendelea na masomo ya sekondari.

Snura ameweka wazi ugumu wa maisha aliyopitia kutokana na kukosa elimu ndio kitu kilichomfanya aweze kuhangaika sana ili wanaye waweze kusoma mpaka elimu ya juu.

Share

Comments

  1. pole dada

  2. bado una nafasi

  3. its never late

  4. take heart

  5. pole

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…

wavatar

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.