Steve Nyerere Athibitisha Kupatana Kwa Wema Na Mh.Makonda

Ikiwa ni siku chache zimepita tangu kuzagae kwa picha zikionyesha msanii wema sepetu na Mh.Paul Makonda  wakiwa pamoja na kwamba wamemaliza tofauti walizokuwa nazo baada ya wema kuamiha chadema na baadae kurudi tena CCM, Steve Nyerere ambae inasemekana kuwa ndiye alifanikisha zoezi la Wema Sepetu kurudi CCM  amefunguka na kuongelea swala la Paul Makonda kumsamehe Wema Sepetu.

Akiongea kwa njia ya simu na GPL, Steve Nyerere ambao alisema kuwa kwa wakati huo alikuwa akitokea Dodoma kuelekea Dar alisema kuwa ni kweli tofauti za wawili hao zieisha na kila kitu kiko sawa sasa hivi wamejikita zaidi katika kujenga taifa na sio kufanya upinzani.

download latest music    

Hakuna uadui wa kudumu katika haya maisha ,isitoshe  wale wote ni vijana wamekutana na kuombana msamaha na mambo yamebaki kuwa historia tu.wanaangalia maisha  mengine ya mbele  kwa sababu safari ni ndefu .Alisema Steve.

Steve anasema kuwa hata kama kulikuwa na tofauti kubwa kati ya wawili hao zilishaisha na ugomvi ule umebaki kuwa historia kwa sababu watu hao wameamua kukubaliana na kuwa kitu kimoja hakuna kilichobaki cha kutenganisha tena.

hili ni funzo kubwa sana hasa kwa wasanii kwamba watu wakogombana wasiongee mambo yote wakamaliza , kuna wasanii watu wakigombana wanaanza kuogea maneno ya  ovyo ovyo  kwa mkuu wa mkoa kupitia kwa wema  sasa leo hao wamepata haya wao sura zao wanazipeleka wapi.-Alifunguka Steve

Hata hivyo kulikuwa na tetesi kuwa mama mzazi wa Wema haonekani nyumbani kwake Sinza Mori na kuwa inawezekana mama  huyo amefichwa sehemu, Steve Nyerere amekanusha habari hizo na kusema kuwa mama huyo yupo nyumbani kwake hakuna alipofichwa kokote.

Nani amekwambia mama hayupo,mama yupo pale pale  na mambo yanaendelea vizuri wala watu hawana haja ya kumtafuta popote-Alimalizia Steve Nyerere

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.