Steve Nyerere: Hukumu Ya Lulu ni Fundisho Kwa Kila Mtu

Muigizaji wa Bongo movie na mwanasiasa maarufu, Steven Nyerere ameibuka na kudai kuwa kilichomtokea muigizaji Lulu Michael ni fundisho tosha kwa wait wote hivyo wajifunze kutokea kwake.

Alipofanya mahojiano na Millard Ayo, Steve Nyerere amefunguka na kusema kuwa kifungo alichopokea Lulu ni fundisho tosha kwa kila mtu hivyo kilichobaki ni kungoja muujiza kama itatokea wa kumuonea huruma na kumuachia huru.

download latest music    

Kusema ulweli nimejisikia huzuni Sana kwa sababu bado ni binti mdogo aliyepita katika misuko suko ya kiutu uzima ambayo hakustahili kwaiyo mimi nimevaa uhusika wa Lulu ili niangalie ingekuwa mimi ningefanyaje lakini nimeishia kuona kuwa hili ni jambo linalo huzunisha sana kwa familia zote mbili lakini kijana wa familia moja ameshapotea hatutamuona tena lakini huyu wa kike na yeye anaenda lupango kwa miaka miwili kitu ambacho sisi kama wananchi hatuwezi kuzuia kwa  sababu mahakama imeshaamua lakini tusiache kumuombea ili Kama itatokea miujiza basi mwenzetu anusurike “.

Lakini pia Steve ameongeza kuwa kesi ya Lulu inatakiwa ichukuliwe mfano kwa vijana wengi ili owe fundisho kwa vitu wanavyofanya kwani kupigana na makosa mengine yanaweza kuwafikisha mbali hivyo ni muhimu kujifunza mapema.

 

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.