Steve Nyerere- Naumwa Sana, Aliyeniroga Anisamehe

January 12, 2018 at 08:06
Steve Nyerere- Naumwa Sana, Aliyeniroga Anisamehe

Msanii mkongwe wa filamu za Bongo movie na mwanasiasa mashuhuri Steve Nyerere ameongea kwa mara ya kwanza baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu na kudai kuwa anaumwa sana na kumsihi aliyemroga amsamehe.

Steve amefunguka na kusema kuwa anasumbuliwa sana maumivu makali kichwani na kwenye miguu yanayomtesa sana. Hivyo anaomba kama kuna mtu yoyote anayemroga amsamehe kwani maumivu aliyonayo ni makali sana.

Loading...

Baada ya habari kusambaa mitandaoni kuwa Steve yuko hoi kitandani haraka sana habari za chini chini za kimbea zilidai kuwa Steve anasumbuliwa Ukimwi jambo ambalo Steve amedai kuwa wanaoendelea kuzusha waendelee tu kwani wanazidi kumpa umaarufu.

Steve amefanya mahojiano na Enews ya East Africa TV na amezidi kufunguk yafuatayo kuhusu maradhi yanayomsumbua:

Nasikia maumivu miguuni na kichwani lakini pia nilikuja kugundulika nina matatizo kwenye upande wa kushoto wa mapafu yangu lakini sahivi miguu hasa ndio bado inanisumbua. Nimeona kwenye mitandao yapo mengi yanayozungumzwa kuna wengine wanadai ni uchawi wengine wanasema nimeathirika na Ukimwi lakini sio mbaya mimi ni staa kwaiyo wacha waseme wanazidi kuniongezea umaarufu na wanataka kujua naumwa nini mimi naumwa miguu na ninachowaambia wanisamehe na kama wapo walinitupia hivo vitu au kuniroga naomba wanisamehe”.

Steve pia amewajia juu waliotangaza habari za yeye kuwa na ngoma kwani hakuna mtu aliyempima mpaka kutia taarifa hizo za uongo lakini pia Steve ameomba watu wamuombee maana gonjwa hill linamsababishia matatizo siyo kwake tu bali hata familia yake maana anashindwa kufanya kazi yoyote.

5
Leave a Reply

avatar
5 Comment threads
0 Thread replies
0 Followers
 
Most reacted comment
Hottest comment thread
1 Comment authors
CeciliaVictoriaJohnsonPatienceWillis Recent comment authors
newest oldest most voted
Willis
Guest
Willis

Acha nawe,karogwa na nani?

Patience
Guest
Patience

Pole sana bro

Johnson
Guest
Johnson

Kafanye uchunguzi wa matibabu

Victoria
Guest
Victoria

Nakutakia nafuu upesi

Cecilia
Guest
Cecilia

Duh! ni huzuni sana


in Entertainment
Loading...

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.